Na Ripota Wetu,Globu ya jamii
NAIBU Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde amefanya ziara ya ghafla kwa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) kwa lengo la kufuatilia maagizo ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambayo aliyatoa Desemba 4 mwaka huu.
Baadhi ya maagizo hayo ni pamoja na uboreshaji wa utoaji wa huduma kwa wawekezaji kupitia Mfumo wa Mahala Pamoja ‘One Stop Facilitaion Centre’, ambapo Waziri Mkuu baada ya kupata maelezo kuna mambo hakukubaliana nayo na hivyo akatoa maagizo.
Hivyo Mavunde amefanya ziara ya ghafla TIC ili kujionea namna shughuli hizo zinavyoendeshwa hasa katika Idara ya Kazi. Akiwa TIC amezungumza na maofisa kutoka Wizara/Taasisi/Idara/Mamlaka mbalimbali wanaotoa huduma kwa wawekezaji ,kupitia mfumo wa Mahala Pamoja na kuwakumbusha kuwa wao ni sehemu ya uchakataji wa vibali na leseni mbalimbali za wawekezaji, hivyo waongeze kasi katika kutekeleza majukumu yao ili huduma husika zipatikane kwa wakati sahihi.
Aidha ,baada ya mazungumzo hayo Mavunde amefanya kikao kazi kati yake na Kamishna wa Kazi Tanzania Gabriel Malata, Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Geoffrey Mwambe na Ofisa Kazi Mfawidhi ndani ya Mfumo wa Huduma za Mahala Pamoja TIC, Emiliana Rweyendela.Ziara ya Naibu Waziri inakuja takribani wiki mbili tangu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipotembelea TIC na kukutana na Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya TIC na kutoa maagizo ya kufanya maboresho mbalimbali ya utoaji wa huduma bora kwa wawekezaji ndani ya Mfumo wa Mahala Pamoja.
Imeelezwa kuwa tangu Waziri Mkuu atembelee TIC kituo hicho chini ya uongozi wa Mkurugenzi Mtendaji kimefanya kikao na Kamishna wa Kazi Tanzania, Kamishna Mkuu wa TRA, Kamishna wa Uhamiaji Tanzania na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kwa pamoja walikubaliana kuboresha mifumo ya utoaji wa vibali, kutoa elimu kwa umma juu ya taratibu zinazotakiwa kufuatwa ili kupata vibali husika na kufanya kazi kama timu ili kushauriana zaidi katika utoaji wa vibali mbalimbali kwa wawekezaji.Pia kama sehemu ya kazi za kila siku, kituo kinaendelea kushughulikia changamoto za uwekezaji kwa kushirikiana na wadau husika ili kufikia lengo la kuwa na mazingira bora ya uwekezaji nchini yatakayowezesha kuvutia uwekezaji zaidi katika sekta mbalimbali kwa manufaa ya Wananchi na Taifa kiujumla.

Weka Maoni yako Hapa
0 comments:
POST A COMMENT