Na Ripota Wetu, Globu ya jamii
MDOGO wake mfanyabiashara maarufu nchini Rostam Aziz, Akram Azizi amehukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kulipa faini ya Sh.milioni 259.5 au kwenda jela miaka 20 jela baada ya kukiri mashtaka 73 ya kukutwa na nyara za Serikali.
Hukumu hiyo imetolewa leo mahakamani hapo ambapo Akram amefanikiwa kulipa faini kwa kulipa fedha hizo, hivyo amekwepa kifungo cha kwenda jela miaka 20 jela.Hata hivyo Mahakama imeamua kuitaifisha nyara hizo na kuwa mali ya Serikali na kuamuru silaha zote ziwe chini ya Polisi hadi mshitakiwa atakapokamilisha taratibu za kisheria za kumiliki silaha.
Akram alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Oktoba 31,2018 akikabiliwa na mashitaka 75 katika kesi namba 82/2018 ikiwemo kukutwa na nyara za Serikali, silaha, risasi na utakatishaji fedha wa dola za Marekani 9,018 lakini kwa mujibu wa sheria alifutiwa mashitaka hayo na kusomewa upya mashitaka 73 ukitoa ya utakatishaji fedha na meno ya tembo.
Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri aliyetoa hukumu hiyo amesema katika mashitaka ya kukutwa na nyama ya nyati, mshitakiwa atatakiwa kulipa faini ya Sh. 43,529,000 na katika makosa 72, yaliyobaki kila moja atatakiwa kulipa Sh milioni tatu.Katika mashitaka hayo 72, jumla ya faini aliyotakiwa kulipa Akram ni Sh.milioni 216. Alisema mshitakiwa akishindwa kulipa faini hiyo atatakiwa kutumikia kifungo cha miaka 20 jela.Awali kabla ya kutolewa hukumu hiyo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Paul Kadushi akisaidiana na Wakili wa Serikali Wankyo Simon aliiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa adhabu kali kutokana na uzito wa makosa hayo ili iwe fundisho kwa wengine wanaofanya vitendo hivyo na kuomba Mahakama itaifishwe nyara zote iwe mali ya Serikali.Hata hivyo mshitakiwa alidai anasumbuliwa na shinikizo la juu la damu na kwamba ni mkosaji wa kosa la kwanza, ana watoto 10 wanaomtegemea
pamoja na mama yake mzazi ambaye ni mzee.

Weka Maoni yako Hapa
0 comments:
POST A COMMENT